Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vichapo vya msuta Wilder kustaafu ngumi

Deontay Wilder Vs Tyson Fury Deontay Wilder

Wed, 5 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Kabla ya kupanda ulingoni kukipiga dhidi ya bondia Zhilei Zhang, Alfajiri ya Jumapili iliyopita, bondia Deontay Wilder alisisitiza kwa tambo nyingi hatapigwa na Zhang na ikitokea akapoteana, ataachana na ngumi kabisa kenye usiku huo uliokuwa na mapambano mengine makali.

Hata hivyo, bondia huyo ameondoka Saudia Arabia lilikopigwa pambano hilo bila kuweka wazi juu ya kauli yake hiyo kama ataitimiza au ataendelea kupanda ulingoni.

Wilder alipoingia ulingoni, alikuwa na imani kubwa sana ya kushinda pambano hilo dhidi ya Mchina huyo ambaye naye pia alichapwa na bondia Joseph Parker.

Katika pambano hilo, lilianza na mambo yalikuwa tofauti kwa Wilder kutokana na makonde mazito mfululizo aliyoyapata kutoka kwa Zhang.

Hata hivyo, raundi ya tano tu, mambo yakawa sio mambo kwa Wilder na alitandikwa ‘vibaya’ na kuanguka chini kama mzigo, kiasi cha mwamuzi kumaliza pambano na hata baada ya Wilder kuinuka, hakuweza kumshawishi mwamuzi kumruhusu aendelee na pambano hilo.

Chanzo: Mwanaspoti