Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vargas ampiga mkwala Khan

16208 Pic+vagas TanzaniaWeb

Sun, 9 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Birmingham, England. Wakati bondia Amir Khan, akisema amepanga kushinda pambano la kesho ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kuwania ubingwa wa Dunia, mpinzani wake Samuel Vargas, kutoka Colombia amepiga mkwala wa mzito, akitamba kumkalisha ndani ya raundi za awali.

Mabondia hao watazipiga kwenye ukumbi wa Arena Birmingham, nchini Uingereza, katika pambano lisilo la ubingwa likiwa la pili kwa Khan, tangu arejee ulingoni, baada ya kujaribu kustaafu na kukaa nje kwa karibu miaka miwili.

"Nimejifua vya kutosha sina sababu ya kuchelea kumshinda, nitalifanya hili kwa sababu ya kutaka kupata nafasi ya kuwania ubingwa wa Dunia,” alisema Khan.

Wakati Khan akiyasema hayo, Vargas, 29, anayeishi Canada alisema hatamuachia Khan aichafue rekodi yake ya ushindi, akiwa ameshinda mapambano 29 sare mawili na kupoteza matatu.

Katika pambano lililopita Khan bingwa wa zamani wa Dunia wa uzani wa super-light, alitumia sekunde 39 kumzimisha Phil Lo Greco kwa KO, pambano lililofanyika Aprili mwaka huu.

Khan alitangaza kustaafu mwaka 2016 baada ya kupigwa bila kutarajia na chipukizi Saul Alvarez ‘Canalo’ katika pambano lililofanyika Mei mwaka huo nchini Marekani.

"Naamini nitamchakaza vibaya Khan sijali uzoefu wake, sitaki kufikiri kuhusu hilo ninachotaka ni ushindi hapo Jumamosi siangalii nitamshinda katika raundi ya ngapi,” alisema Vargas.

Kocha mpya wa Khan, Joe Goossen, alisema kwa jinsi walivyopfanya maandalizi hana wasiwasi kuwa atamshinda mapema mpinzani wake.

Chanzo: mwananchi.co.tz