Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Kuwaona Mwakinyo, Tinampay kiingilio bure Uwanja Uhuru

Sun, 24 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mabondia Hassan Mwakinyo na Arnel Tinampay wamekutana kwa mara kwanza mbele ya mashabiki kwenye viwanja vya Leaders na kutangaza pambano lao halitakuwa na kiingilio.

Mabondia hao wapatamba ulingoni Novemba 29, katika pambano hilo la raundi 10 la uzani wa welter litapigwa kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mabondia hao leo Jumapili wamekutana uso kwa uso ikiwa ni siku nne kabla ya kupanda ulingoni, hakutakuwa na kiingilio.

Bondia Mwakinyo amesema aliomba pambano hilo lisiwe na kiingilio ili kutoa fursa kwa mashabiki wengi kujitokeza kumshuhudia.

"Tulijadiliana pambano lisiwe na kiingilio ili kuwapa fursa mashabiki wengi kujitokeza kulishuhudia, ombi langu limekubaliwa hivyo pambano langu halitokuwa na kiingilio," alisema Mwakinyo.

Alisema hata hivyo kutakuwa na utaratibu maalumu wa watu watakaokaa jukwaaa kuu na kawaida kuingia uwanjani ili kuweka utaratibu mzuri ambao hautaibua vurugu.

Pia Soma

Advertisement
Promota wa pambano hilo, Jay Msangi alisema mashabiki elfu 20 pekee ndio wataruhusiwa kuingia uwanja wa Uhuru kulishuhudia pambano hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz