Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usyk aacha pambano lake na Joshua, ashika bunduki

USYK.png Bondia Oleksandry Usyk wa katika akiwa ameshika silaha lindoni

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Bondia bingwa wa uzito wa juu Duniani Oleksandr Usyk amesema hajui ni lini atapanda ulingoni kutetea ubingwa wake wa uzito wa juu wa dunia dhidi ya Anthony Joshua katika pambano lao la marudiano lililopangwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu 2022.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 35 amerudi kuungana pamoja na majeshi ya nchi yake na kujiunga na kambi ya Kyiv Territorial Defense katika harakati za kulinda nchi yao kufuatia uvamizi wa Urusi.

Usyk alikuwa nchini England wiki iliyopita akiwa na mazungumzo na Joshua kuhusu pambano la marudiano baada ya kumvua ubingwa wa dunia wa uzito wa juu wa IBF, WBA na WBO mwezi Septemba mwaka jana. Lakini sasa Usyk amerejea nchini kwao Ukraine katika jiji la Kyiv kushika silaha na kuilinda nchi yake akidai nchi yake ni muhimu sana kuliko mikanda hiyo ya masumbwi kwa sasa.

Bondia huyo namba moja duniani wa uzito wa juu na kuwa Unified Heavy Weight Champion anaungana na mabondia mabingwa wa zamani wa uzito wa juu wa nchi yao ya Ukraine, Vitali na Wladimir Klitschko kwenye umoja wa majeshi ya Kyiv Territorial Defense kwa ajili ya mapambano ya kivita ya kujihami dhidi ya Urusi huku akisisitiza mapatano ya amani na rais Vladimir Putin wa Urusi.

Chanzo: eatv.tv