Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usky ampigia hesabu mpya Joshua

Anthony Joshua Vs Olexandr Usyk S0kyjciajksg1waqhpx64m82g Usky ampigia hesabu mpya Joshua

Tue, 30 Jul 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bondia bingwa wa kwanza asiyepigika (undisputed) karne ya 21, Oleksandr Usyk hana wasiwasi na pambano la marudiano dhidi ya Tyson Fury, kiasi cha upande wake kuanza kupanga mkwanja gani atavuna akizichapa tena Anthony Joshua.

Akiwa ametoka kushinda kwa pointi pambano la mwezi Mei dhidi ya Tyson Fury, Usyk alijibu mapigo ya Fury, pambano hilo la kwanza lilikuwa rahisi kiasi cha kutokubaliana na matokeo ya ushindi alioupata akimuahidi urahisi huo kwenye pambano la marudiano Desemba, mwaka huu.

Ni uhakika huo alionao Usyk kumchapa tena Fury kwenye pambano hilo, promota wake Alexander Krasyuk ameweka wazi kuanza mipango ya kupigana pambano la tatu dhidi ya Joshua, wakitarajia atamchapa Daniel Dubois ili waketi mezani kuzungumzia dili la pambano namba tatu la mabondia hao.

Kutokana na kutambua upande wa Joshua ‘AJ’ unatamani sana kupata nafasi ya kupigana tena na Usyk, Krasyuk alifichua uwepo wa mpango wa kuweka dau nono la kufanikisha pambano namba tatu, lengo likiwa ni Dola 200 milioni ili wazichape upya kutokana na thamani kubwa aliyonayo AJ ambayo imeongezwa na kushinda kwake mapambano matatu ya mwisho pamoja na uwezekano wa kumshinda Dubois, mwezi Septemba.

Chanzo: Mwanaspoti