Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usiku wa nani kuwa mrefu? Kidunda au Katompa?

Katompa Mabondia watakaooneshana ubabe ulingoni usiku wa leo

Sun, 26 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Leo Jumapili ya Disemba 26, ni siku kubwa na maalumu kabisa kwa wapenzi wa michezo hususani mchezo wa masumbwi Tanzania na Afrika mashariki na kati kwa ujumla wake.

Kushuhudia pambano la funga mwaka kuwania ubingwa wa Vacant WBF Super Middleweight (Kg 76) kati ya mtanzania Seleman Kidunda vs Tshimanga Katompa kutoka DR Congo.

Katompa ambaye siku chache zilizopita aliapishwa kuwa mwanasheria baada ya kuhitimu shahada ya mafunzo ya sheria katika chuo kikuu cha mjini Kinshasa, alianza kucheza ngumi za kulipwa Februari 2012, akimshinda Salumu Chance kwa pointi.

Ni bondia mwenye nyota mbili, akishika nafasi ya 1 DR Congo, afrika nafasi ya 9, nafasi ya 155 duniani, hii ni kwa mabondia wa daraja la uzito anaochezea (Super Middleweight Kg 76).

Tangu mwaka 2018 Katompa hakuwa amecheza pambano lolote, kabla ya Oktoba 9 mwaka huu kuibuliwa na Promota Siraju Kaike kucheza na Dullah Mbabe.

Katika pambano la 'KIBOKO YA WAGENI', ambapo Katompa alishinda kwa pointi za majaji wote (UD) na ndio pambano lake la mwisho kabla ya kuvaana na Kidunda.

Kwa upande wa mwenyeji Seleman Kidunda ambaye ni mtumishi wa jeshi la wananchi Tanzania, alianza ngumi za kulipwa mwezi Juni mwaka 2019, baada ya kufanya unyama mkubwa na kutikisa kwenye ngumi za ridhaa.

Pambano lake la kwanza alicheza dhidi ya Karage Suba, ambapo alishinda kwa TKO, kutoka mwaka 2019 hadi leo 2021 amecheza jumla ya mapambano 7 pekee wastani wa mapambano 2 kila mwaka, akishinda yote 7 kwa KO na TKO.

Kidunda ni bondia mwenye nyota moja na nusu, anashika nafasi ya 3 Tanzania, Nafasi ya 19 Afrika na Nafasi ya 268 kidunia, hii ni kwa mabondia wa daraja la uzito anaochezea (Super Middleweight Kg 76).

Pambano la mwisho kabla ya kumvaa Katompa leo, alicheza Oktoba 30 mwaka huu pale alipomchapa kwa KO bondia Jacob Maganga wa Tanzania.

Mabondia wote wawili ni UNBEATEN, Je, Ni Kidunda ataendeleza rekodi yake ya kushinda kwa KOs au ataootea?, Na je, Katompa ataendeleza rekodi ya kuwachapa mabondia watanzania?.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live