Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unamkumbuka Lewis vs Evander? Soma hapa

GettyImages 51533652 770x491 Unamkumbuka Lewis vs Evander? Soma hapa

Tue, 23 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Ikiwa imepita takriban miaka 25 tangu lilipopigwa pambano la kibabe la uzito wa juu duniani nchini Marekani kati ya Lennox Lewis Evander Holyfield, sasa linarudi buana.

Itakumbukwa kwamba katika pambano hilo lililopigwa Machi 13, 1999 kwenye Ukumbi wa Madison Square Garden, New York, Marekani, Holyfield alichapwa na Lewis kwa pointi za majaji wawili kati ya watatu, ambapo ni mmoja tu aliyewapa alama sawa, Larry O'Connell 115-115 huku Stanley Christodoulou akimpa Lewi 116 dhidi ya 113 na Eugenia Williams 115-113.

Hata hivyo, pambano hilo lililalamikiwa sana na mashabiki waliohudhuria na walioliangalia kupitia televisheni wakiamini kwamba Holyfield aliyekunja mkwanja wa Dola 20 milioni alimchapa Lewis aliyeingiza Dola 10 milioni.

Wababe hao waliostaafu masumbwi kwa sasa walizichapa ili kuunganisha mikanda ya ubingwa waliyokuwa wakiishikilia kutoka katika mashirikisho matatu ikiwa ni ile ya WBA na IBF aliyokuwa nayo Evander huku Lewis akiwa nao ule wa WBC.

Februari 17, 1999: Evander Holyfield (kulia) akizichapa na Lennox Lewis

Hata hivyo, achana na pambano hilo, kwani wiki chache zijazo kuna kitu cha la aina hiyo kitapigwa kutoka kwa mabondia wa kisasa, Tyson Fury na Oleksandr Usyk watakapopanda ulingoni katika Ukumbi wa Kingdom Arena mjini Riyadh, Saudia Arabia kusaka mbabe baina yao.

Katika pambano hilo lililopangwa kupigwa Februari 17, dunia inaweza kushuhudia kwa mara nyingine maajabu ya aina yake pengine kama yale yaliyotokea miaka 25 iliyopita au zaidi ya hayo pale wababe hao watakapokutana ulingoni.

Siku hiyo wababe hao wawili wasiopigika kwenye uzito wa juu ambao wanashikilia mikanda hiyo kwa sasa watakuwa wakisaka rekodi na utajiri wa kipekee kwani wamewekewa mezani zaidi ya Dola 300 milioni ili kuzichapa.

Na ili kuthibitisha kati yao nani atakuwa bondia asiyepigika (undisputed) wote hakuna aliyewahi kupigwa kwani Fury ana rekodi tamu ya kushinda mapambano 34, sare moja na hajapigwa katika pambano lolote ilhali Usyk ameshinda mapambano 21 aliyopigana tangu alipoanza kupigana ngumi. Je ni nani atapigwa kati yao? Kaa mkao kwani Februari 17 siyo mbali.

Chanzo: Mwanaspoti