Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ubabe kwa Mwakinyo, Kiduku, Mfaume hawatoboi!

Mwakinyo Pic Data Ubabe kwa Mwakinyo, Kiduku, Mfaume hawatoboi!

Tue, 27 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

NAMBA hazidanganyi! Ndivyo ilivyo kwa bondia Hassan Mwakinyo ambaye ubora wake unawafunika mastaa watano wa ndondi nchini hata wakiamua kuungana bado hawafui dafu.

Mwakinyo bondia wa nyota tatu anayepigania uzani wa super welter ndiye kinara kwa mabondia wa kila uzani ‘pound for pound’ nchini.

Mtandao wa ngumi za kulipwa unamtaja Mwakinyo kuwa bondia namba moja nchini mwenye pointi 9.931.

“Ili uvune pointi nyingi inategemea na aina ya bondia unayepigana naye, si ilimradi umepigana na kushinda basi unapanda,” anasema rais wa Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), Agapeter ‘Mnazareth’ Basil.

Anasema kinachoangaliwa katika kuongeza pointi za bondia ni ubora wa mpinzani wake na alikuwa na pointi ngapi kabla ya pambano.

“Ndio sababu mabondia wasiokuwa na majina wanang’angania kucheza na mabondia wenye majina kwa kuwa wanafahamu wanachokitaka ni pointi. Wenye majina wanapokubali ni kama wanacheza pata potea kwa kuwa hata wakishinda haiwasaidii, tatizo ukipigwa ndiyo inakuwa kama kilichotokea kwa Mwakinyo Uingereza,” alisema Agapeter na kuongeza;

“Alimchapa kwa TKO aliyekuwa bondia namba nane wa dunia, Sam Egginton, pambano lililompandisha kutoka nafasi ya 179 hadi ya 14 duniani, ingawa sasa ni wa 49 kwenye uzani wake. Kinachotokea, bondia yeyote akienda kupigana nje ya nchi mara nyingi wanamtegemea kupigwa, kushinda kwake uwa hawalioni, ikitokea umeshinda unajisafishia njia na ndivyo ilikuwa kwa Mwakinyo.”

MBABE, KIDUKU WANASUBIRI

Mabondia wengine wenye majina kama Twaha ‘Kiduku’ Kassim, Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’, Mfaume Mfaume, Mada Maugo na Japhet Kaseba kama wataunganisha pointi zao, bado hawafui dafu kwa Mwakinyo.

Boxrec inamtaja Mwakinyo kuwa na pointi 9.931 na nyota tatu, tofauti yake na Saul Alvarez bondia namba moja wa dunia ni pointi .... na nyota ....

Kibongo bongo, Mwakinyo kawaacha mbali mabondia wengi, ukimuondoa Ibrahim Class bondia namba mbili kwa ubora ambaye ana pointi 7.378 wengine wengi baadhi wakiwa na majina hawampati Mwakinyo hata wakiunganisha pointi zao.

Miongoni mwao ni Kiduku mwenye pointi 3.030, Mbabe ana 1.352,Mfaume .145, Maugo .072 na Kaseba.010, ambazo zikijumlishwa zinafika pointi 4.609, wanaachwa kwa pointi 5.322 na Mwakinyo.

KINACHOWAKWAMISHA WENGINE

Wakati Mwakinyo akiendelea kuchanja mbunga, mdau wa ngumi nchini, Chata Michael anasema, tatizo kubwa ni mabondia wengi nchini kuamini nje ya nchi hakuna ushindi.

“Wanapopata nafasi ya kucheza na mabondia wakubwa, hawaitumii, vema, tofauti na Mwakinyo ambaye ni bondia anayechungulia mapambano.

“Nafikiri pia menejimenti yake iko vizuri katika kumshauri, hasa promota wake, Ally Mwazoa,” anasema mmoja wa wadau wa ngumi, Chata Michael.

Mwazoa anasema hata bondia huyo alipoletewa ofa ya kuzichapa na Eggington, hawakuwa na papara waliangalia ni bondia yupi atawanufaisha.

“Tulikuwa na ofa tatu, nikamwambia Mwakinyo nenda kacheze na Eggington, huko hata tukipigwa hatuna hasara, lakini kwa nini upigwe? nenda kasimame upigane, akanielewa na ndilo pambano limempa pointi nyingi,” anasimulia.

Mwazoa anasema kuna watu uwa wanawapeleka mabondia nje ili wapigwe na nyota zao na pointi zinachukuliwa, hiyo ni changamoto.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz