Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson haogopi kuzipiga na Jake

Tyson Haogopi Kuzipiga Na Jake Tyson haogopi kuzipiga na Jake

Thu, 4 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa Mike Tyson ambaye anatarajia kuzichapa mwezi Julai mwaka huu na bondia chipukizi Jake Paul, amefunguka kuhusu hofu yake na jinsi anavyoweza kukabiliana nayo.

Katika mahojiano yake ya hivi karibuni na Sean Hannity, Tyson alieleza kuwa haogopi pambano lake na #Jake kwani huwa anachokiogopa ndicho anachikifanya, huku akiweka wazi kuwa aliwahi kuogopa pambano moja tuu la #Roy ambalo alizichapa na Jones Jr mwaka 2020.

Aidha #Mike aliendelea kwa kueleza kuwa kwa sasa anachokiogopa ni kifo tu na siyo pambano lake lolote, hivyo basi yupo tayari kuzichapa na Jake.

Tyson (57) anatarajia kuingia ulingoni na Jake Paul (27) katika uwanja wa AT&T uliopo jijini Texas pia pambano hilo litaonesha Mubashara (live) kupitia #Netflix.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live