Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson asema amechanja corona bila hiari

Tysonpic Bingwa wa zamani wa uzito wa juu, Mike Tyson

Sat, 9 Oct 2021 Chanzo: mwananchi

Gwiji wa zamani wa ngumi za kulipwa, Mike Tyson amepata chanjo dhidi ya ugonjwa wa virusi vya corona, Covid-19, lakini amesema hakufanya hivyo kwa hiari akieleza kuwa umuhimu kusafiri ndio umemlazimisha.

"I didn't do it willingly," Tyson alisema bondia huyo mwenye miaka 55 akikaririwa na tovuti ya Washington Examiner Jumanne.

"Nina woga kidogo na hilo. Nilijikuta nalazimika kusalimu amri kwa sababu nina safario kimataifa. Na kama sisafiri, hatuli."

Bondia huyo aliyetamba katika ngumi za uzito wa juu duniani aliwahi kuambukizwa Covid-19 wakati wa janga hilo, lakini anasema anajisikia vizuri kwa sasa.

"Naweza kuwa niliupata, lakini najisikia vizuri sasa," tovuti hiyo inamkariri Tysion alipoongea na gazeti la USA Today Sports katika mahojiano yaliyofanyika katika ofisi za kampuni yake inayojihusisha na biashara ya bidhaa zitokanazo na bangi.

"Najisikia vizuri kuliko wakati mwingine wowote."

Chanzo: mwananchi