Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Fury amchapa Wilder kwa KO

Pjimage (36) Fury akimgaragaza Wilder

Sun, 10 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia kutoka nchini Uingereza Tyson Fury, kwa mara ya tatu ameibuka mbabe mbele ya Bondia hatari na mwenye tambo nyingi kutoka nchini Marekani Deontay Wilder

Tyson Fury amefanikiwa kutetea mkanda wa WBC na The Ring kwa kumchakaza Deontay Wilder kwa KO, asubuhi ya leo Jumapili.

Hiyo ilikuwa mara yao ya tatu wamekutana, lakini Fury ameshinda mara mbili na sare moja.

Ulingo wa T-Mobile Arena uliopo Las Vegas ndiyo uliotumika kumlambisha sakafu Wilder katika raundi ya 11 baada ya kupigwa konde kali la mkono wa kulia na kwenda chini mzimamzima.

Fury au The Gypsy King, alimchakaza mpinzani wake huyo kwa jina la utani la Bronze Bomber baada ya kuonekana kuchoka zaidi kila muda ulivyokuwa ukisonga mbele katika pambano hilo.

Katika pambano hilo ngumi 148 zimetua kwa Wilder dhidi ya 72.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live