Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Fury alipata majeraha mabaya kabla ya ushindi wake na Wilder kwa mara ya pili

 121501297 Tysonfury Bondia Tyson Fury akiwa amemuangusha wilder katika Pambano lao la mara ya mwisho

Wed, 10 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa wa uzito wa juu kutoka nchini Marekani, Bondia Tyson Fury alifanyiwa upasuaji katika maungio yake ya mikono (viwiko) baada ya kupata majeraha mabaya kabla ya ushindi wake wa mara ya pili dhidi ya Deontay Wilder, amesema baba wa Tyson, John Fury.

Tyson mwenye umri wa miaka 33 aliibuka kidedea katika raundi ya 11 dhidi ya mmarekani huyo na kutetea mkanda wake wa WBC October mwaka huu huko Las Vegas.

"Tyson alipata majeraha mabaya sana kuelekea mchezo ule," John Fury amekiambia kituo cha BT Sport.

"Alikua na matatizo tangu mwanzo wa mchezo, si ndivyo?"

Tyson Fury aliangushwa mara mbili katika raundi ya nne, kabla ya kumbadilishia kibao mpinzani wake na kumchapa raundi ya 11 na kubaki kama bondia asiepigika na bingwa wa dunia wa uzito wa juu.

"Kijana wangu ndio namba moja kwa sasa, mtu ambae ataacha alama na atazungumzwa kwa miaka mingi ijayo" ameongeza John Fury

Chanzo: www.tanzaniaweb.live