Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Fury afikiria kustaafu ngumi 2022

Tyson Fury 33 Tyson Fury bingwa wa uzito wa juu wa Dunia mara mbili kwa sasa anamiliki mkanda wa WBC

Wed, 2 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Bondia wa uzito wa juu raia wa Uingereza Tayson Fury amesema anaweza kustaafu kucheza masumbwi baada ya pambano lake dhidi ya bondia Mwingereza Dilian Whyte litakalofanyika Aprili 23 mwaka huu.

Fury amesema hayo baada ya kuulizwa kama atastaafu baada ya pambano lake na Whyte alipoulizwa kwenye mkutano na waandishi wa habari wakati wakufanya promosheni ya pambao hilo,

“Ndio Kwa asilimia 100%. Mimi ni bingwa wa dunia mara mbili asiyepingwa. Nina pauni milion 150 kwenye akaunti yangu ya benki (zaidi ya bilioni 461 kwa pesa za kitanzania ) na hakuna chochote cha kuthibitisha kwa mtu yeyote." Amesema Fury.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 33 atakuwa na kibarua cha kuutetea mkanda wake wa WBC kwenye pambano hilo la uzito wa juu Heavyweight litakaofanyika katika uwanja wa Wembley jijini London Aprili 23, 2022.

Tyson Fury amepigana mapambano 32 ameshinda mara 31 ametoka sare pambano 1 huku mapambano 22 ameshinda kwa KO. Na mpinzania wake Dillian Whyte ambae pia ana umri wa miaka 33 amepigana mapambano 30, ameshinda 28 kapigwa mara 2 na mapambano 19 ameshinda kwa KO.

Chanzo: eatv.tv