Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Fury, Oleksandr Usyk rasmi ulingoni

Usyk Vs Tyson Fury Mabondia Tyson Fury na Oleksandr Usyk

Wed, 21 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya kutawala kwa tetesi tu, sasa imekua rasmi, ulimwengu unaenda kupata bingwa asiyepigika (undisputed) katika mchezo wa masumbwi, ambaye hatimaye atashikilia mikanda minne ya uzito wa juu (heavyweight) kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20.

Bondia mmojawapo atakayefanikiwa kuibuka bingwa wa mikanda hiyo ni Tyson Fury au Oleksandr Usyk ambao wote wawili wanashikilia mikanda yote minne ya uzito wa juu duniani ambayo ni WBC, WBA, WBO na IBF mtawalia.

Muingereza Tyson, anashikilia mkanda wa WBC alioutetea dhidi ya Derek Chisora mapema mwezi huu, wakati mpinzani wake kutoka Ukraine, Usyk anashikilia mikanda ya WBO, WBA na IBF aliyoitetea dhidi ya Anthony Joshua katikati ya mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live