Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Fury: Nitamfungia Tommy ndani akishindwa dhidi ya Paul

FURY FAMILY Tyson Fury na Tommy Fury

Thu, 11 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tyson Fury amemwambia mdogo wake Tommy Fury kuwa iwapo atapoteza pambano lake dhidi ya Jake Paul atamfungia ndani asisherekee sikuku ya krismasi.

Tyson ni bingwa wa dunia wa uzito wa juu kwenye mchezo wa masumbwi, alizungumza na waandishi wa habari siku ya jana akihamasiaha kuhusu pambano hilo ambalo litakwenda kuchezwa kwenye ukumbi wa Amalie Arena jijini Florida disemba 18 mwaka huu.

Tyson anaamini mdogo wake atashinda kwenye mtanange huo, kuwa Paul litakuwa pambano lake la kwanza kupoteza kwenye mikono ya Tommy.

“Nadhani litakuwa pambano zuri kwa kila mtu ambaye atakwenda kuangalia, duniani kuna watu wengi wanavutiwa kuangalia pambano hili.”

“Linawakutanisha vijana wawili, ambao hawajapoteza, nalisubilia, utakuwa usiku mzuri sana, nafikili Tommy atampiga, sijamvunjia heshima Jake Paul, lakini kama nilivyosema awali kwa Tommy, ikiwa atashindwa kumpiga Paul, atafute nchi ya kwenda na akakae huko asirudi.” amesema Tyson Fury.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live