Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tyson Ataja Kiasi kuzichapa na Jake Paul

Paul Jake P Jake Paul

Sat, 26 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Gwiji wa ndondi Mike Tyson amefunguka kiasi anachoweza kuchaji kama mapromota wakitaka pambano lake na Youtuber Jake Paul litokee.

Aliombwa kutaja kiasi cha pesa ambayo itamshawishi mwanamasumbwi huyo kurejea ulingoni akiwa na umri wa miaka 55 kwaajili ya kuchapana na Jake Paul na Tyson alidai kiasi cha dola bilioni moja inaweza kumrudisha ulingoni.

“Daima nimekuwa nikivuta sigara naye,” Tyson alisema kwenye podikasti yake, inayoitwa Hotboxin.

“Nilikuwa naye huko St. Barts muda mfupi uliopita, tukifanya sherehe.

“Hakuna mtu aliyeniambia kuwa nitakuwa na pambano na Paul.

“Sijawahi kusikia kuhusu hili ndo nasiki kutoka kwenu jamani tuna mengi zaidi macho ya blu na nywele za blonde hivyo vitu ni gharama, tuna hitaji kutengeneza pesa aisee.

“Hana pesa za mfalme. Kwa hiyo mkataba wa mfalme uko wapi?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live