Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha kiduku afunguka alivyopigwa mpaka akaona giza

Twaha Kiduku (1).jfif Twaha kiduku afunguka alivyopigwa mpaka akaona giza

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa Kimataifa kutoka Tanzania, Twaha Kiduku ambaye juzi alishinda Ubingwa wa Afrika/Mabara (UBO Intercontinental Super middle weight) amefunguka namna alivyopigwa nchini Zambia na kupoteza uwezo wa kuona akiwa ulingoni.

Juzi, Twaha kiduku alishinda kwa pointi baada ya kumtwanga Bondia Abdo Khaled kutoka nchini Misri katika pambano la raundi 10 lililopigwa Mkoani Mtwara.

"Nilienda kupigana Zambia na Mbea Kangu, round ya tatu (3) alinipiga ngumi nikawa naona giza sioni mtu, nikawa najifanya kama namuona lakini nilikua simuoni , ila baada ya muda nikamuona na nilifanikiwa kumpiga mpaka akazimia "- Kiduku

Aidha, Kiduku amesema kuwa jina lake halisi ni Twaha Kassim, lakini jina la Twaha Kiduku limetokana na mtindo wake wa nywele ‘style ya Kiduku.’

Akizungumzia namna alivyoingia katika Masumbwi akiwa bado Mwanafunzi, Kiduku amesema; "Kabla sijawa Bondia nilikua najiuliza Mabondia wanapigana Hasira wanazitolea wapi?

"Siku moja Fransis Cheka alikua anapita mitaa ya Morogoro watu wakawa wanamshangilia, ndo nikautamani zaidi mchezo wa ngumi.

"Nilitamani sababu nilikua mtundu na nilikua napenda niogopeke hata Shuleni nilikuwa nikiingia nachukua Shilingi tano (5) za watoto wenzangu," amesema Kiduku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live