Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku kufia ulingoni leo

Twaha Kiduku Morogoro Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’ amesema yuko tayari kumchakaza mpinzani wake katika pambano la kimataifa la kuwania mkanda wa dunia wa WBF dhidi ya bondia kutoka Agentina, Hugo Victor kwenye Uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro leo.

Akizungumza jana nyota huyo alisema amejipanga vizuri na anamheshimu mpinzani wake akijua wazi hapaswi kumbeza ila atahakikisha hawaangushi mashabiki wake.

“Nimefanya maandalizi ya kutosha kuhakikisha nawapa raha mashabiki wangu, naomba mjitokeze kwa wingi kwenye Uwanja wa Jamhuri na mimi sitawaangusha,” alisema Kiduku. Kiduku amekuwa kwenye kiwango bora tangu mwaka jana ambapo katika mapambano matatu aliyocheza mfululizo hajapoteza.

Mara ya mwisho alicheza na bondia kutoka Misri, Abdo Khaled Machi mwaka huu mkoani Mtwara na kuibuka ushindi. Pambano lingine litawahusisha mabondia Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ dhidi ya Limbani Lano kutoka Jeshi la Malawi badala ya Mbiya Kanku wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) aliyetangazwa awali.

Dulla Mbabe anatakiwa kuwathibitishia Watanzania kuwa sasa amerudi upya baada ya kufanya vibaya katika pambano lake la mwisho la kimataifa dhidi ya bondia kutoka DRC, Erick Katompa.

Akizungumzia pambano hilo, Dulla Mbabe alisema amekuwa na bahati mbaya ya kubadilishiwa mabondia kuelekea dakika za mwishoni na mwaka jana ilitokea kama ilivyo sasa lakini kwa sasa hana hofu amejiandaa vya kutosha na yuko tayari kupambana na yeyote.

Mapambano mengine ya utangulizi yatakuwa ni Karim Mandonga dhidi ya Said Mbelwa, Issa Maneva dhidi ya Oscar Goba na Magambo Christopher dhidi ya Juma Misumari.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live