Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku asisitiza ushindi Desemba 26

Twaha Kiduku (1).jfif Twaha Kiduku asisitiza ushindi Desemba 26

Wed, 13 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Bondia Ngumi za Kuliwa Twaha Kassimn Kiduku, amesema anaendelea kujifua chini ya Kocha wake Pawa Iranda, ili kuhakikisha anashinda pambano dhidi ya Mohamed Sebyala kutoka Uganda.

Kiduku atavaana na Sebyala Desemba 26, mwaka huu katika pambano la raundi 10 lisilo la ubingwa litakalofanyika katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, jijini Dar es salaam.

Akizungumza mjini Morogoro, Kiduku amesema kocha wake, Pawa Iranda amekuwa akimpatia mbinu bora zitakazomuwezesha kumchapa mpinzani wake.

“Naendelea kujifua kwa lengo la kumkabili mpinzani wangu Sebyala, lakini Mashabiki na Watanzania wategemee burudani nzuri kutoka kwangu kwa sababu naendelea kunolewa na kocha wangu Iranda,” amesema Kiduku.

Kwa upande Kocha Iranda, amefichua kuwa Twaha Kiduku ameendelea kuimarika na anaamini Bondia wake atafanya vyema katika pambano hilo la Kimataifa.

“Nimekuwa nikimpatia mazoezi mbalimbali ikiwemo ya kuongeza pumzi na stamina, lengo ni kumweka fiti kwa pambano na atafanya vyema,” amesema.

Twaha Kiduku ataingia katika pambano hilo akiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa pointi dhidi ya Asemahle Wellem kutoka Afrika Kusini, katika pambano lililofanyika Julai 30, mwaka huu jijini Mwanza.

Chanzo: Dar24