Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku amchapa Dullah mbabe, abeba Crown mpya

BONDIA TWAH Twaha kiduku (kushoto) akimsukumia ngumi Dulla Mbabe

Sat, 21 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hatimaye ule usiku wa deni uliokuwa ukisubiriwa na wengi umefika na mbabe baina ya mabondia wawili waliotambiana kwa muda mrefu kapatikana na ni kutokea kule Mji kasoro bahari.

Twaha Kiduku kutokea Morogoro ameshinda gari aina ya Toyota Crown Athlete baada ya kushinda pambano la raundi 10 kwa pointi dhidi ya Dulla Mbabe.

Pambano hilo lililokuwa linasubiriwa kwa hamu kutokana na tambo za mabondia hao limefanyika Ubungo Plaza jijini Dar es Salaam, huku idadi kubwa ya watu wakijitokeza kuwashuhudia wababe hao.

Pambano hilo lililoanza majira ya saa sita za usiku lilishuhudia almanusura liishie raundi ya kwanza baada ya Dulla mbabe kumsukumia konde zito la mkono wa kulia Twaha na kumsababisha aende chini kabla ya mwamuzi Pendo Njau kumuhesabia twaha ili kujua kama anaweza kuendelea ama la, lakini aliinuka na kuendelea.

Katika raundi zote zilizofuata Twaha Kiduku alitawala mchezo hivyo mpaka mwisho majaji wote watatu walitoa 98-91,98-91,98-91 hivyo Twaha Kiduku akaibuka mshindi wa Pambano hilo kwa point.

Pambano hilo la Uzito wa Middle Super Weight lilikua ni la kumaliza utata kati ya mabondia hao wawili wa kujua nani mbabe kati yao lakini ni dhahiri kuwa Twaha Kiduku ameshindikana hasa baada ya kumpiga Dulla kwa mara ya pili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live