Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku: Nitajirekebisha 2024

Twaha Kiduku Morogoro Twaha Kiduku

Thu, 28 Dec 2023 Chanzo: Dar24

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini Tanzania, Twaha Kassim ‘Twaha Kiduku’ amesema atarekebisha makosa madogo yalitokea katika pambano lililopita dhidi ya mpinzani wake kutoka nchini Uganda Mohamed Sebyala.

Twaha Kiduku ambaye alifanikiwa kutetea ubingwa wake wa PST kupitia pambano hilo lililopigwa katika Ukumbi wa Ubungo Plaza, amesema alishindwa kumpiga mpinzani wake KO, kutokana na ugumu, ubora na uzoefu aliokuwa nao bondia huyo.

“Nawaomba Watanzania waendelee kunisapoti kwani nimeona kuna mapungufu madogo madogo ambayo nitayafanyia kazi kuhakikisha ninatoa burudani kwa mashabiki wangu,” amesema Kiduku.

Bondia amesema huyo moja ya mipango na mikakati yake ya mwakani kufanya vizuri katika mapambano yake na kuonyesha ubora wa pekee kwa lengo la kuwapa furaha mashabiki zake.

“Ofa zinakuja nyingi kwangu, lakini uongozi wangu unaangalia pambano lenye maslahi kwangu, siyo nipigane bila mpangilio kwa sababu hii ni kazi kwangu yangu, ninatarajia kufanya mambo makubwa zaidi na kutoa burudani ya aina yake kwa mashabiki wangu katika mapambano ya mwakani,” amesema.

Chanzo: Dar24