Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Twaha Kiduku: Nipo tayari, Sitawaangusha

Twaha Kiduku T Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’

Fri, 25 Mar 2022 Chanzo: dar24.com

Bondia Twaha Kassim ‘Kiduku’ amewatoa hofu Mashabiki wake kuelekea pambano la kesho Jumamosi (Machi 26), ambalo litamkutanisha na Bondia kutoka DR Congo Alex Kabangu.

Twaha Kiduku atapanda ulingoni katika ardhi ya Morogoro kwa mara ya kwanza baada ya miaka kadhaa kupita, ambapo asilimia kubwa ya mapambano yake amekua akitamba akiwa jijini Dar es salaam.

Bondia huyo ambaye anakumbukwa kwa kumchakaza Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ amesema yupo tayari kwa pambano hilo, baada ya kufanya maandalizi kabambe kwa zaidi ya miezi miwili.

“Niko sawa, niko powa kabisa napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa hilo, hadi sasa pambano letu lipo katika hatua za mwisho baada ya taratibu zote kufuatwa na kukamilishwa, Mashabiki wangu ninatarajia kutowaangusha na ninaamini hilo linakwenda kutokea.”

“Njooni kwa wingi hapa Morogoro ili mshuhudie namna bondia wenu anavyopambana ili kuipa heshima nchi ya Tanzania, nimejiandaa vizuri sana, nipende kuwatoa hofu kwa hilo.

Leo Ijumaa mabondi hao wamepima uzito Mkoani Morogoro tayari kwa kukutana uso kwa macho kesho Jumamosi (Machi 26).

Chanzo: dar24.com