Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tony Rashid amzimisha Mahlangu

Radhi Tony Tony Rashid akitangazwa bingwa

Sat, 26 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Mtanzania, Tony Rashid amemchapa Bongani Mahlangu kutoka Afrika Kusini kwa pointi kwenye pambano la raundi 12 lililopigwa usiku wa kuamkia leo. Ushindi ambao umempa mkanda wa ABU.

Ikumbukwe kuwa, katika pambano la kwanza Mahlangu amchapa Tony kwa KO katika raundi ya mwisho licha ya Tony kuonekana kucheza vizuri kuanzia raundi ya kwanza akimpoteza vibaya mpinzani wake lakini raundi ya 12 alipigwa na kuvuliwa mkanda huo.

Pambano la jana lilikuwa la kisasi ambapo mambondia wote walicheza vizuri tena kuanzia raundi ya kwanza huku Tony akionekana kuzisoma vizuri mbinu za mpinzani wake na kufanikiwa kumchapa kwa pointi na kurejesha mkanda wake wa ABU.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live