Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania yajihakikishia Medali mbili ndondi All African Games

Dhuf.jpeg Tanzania yajihakikishia Medali mbili ndondi All African Games

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Ezra Paul Mwanjwango wa Tanzania amefanikiwa kutinga Nusu Fainali katika Michezo ya Afrika (All African Games) inayoendelea nchini Ghana baada ya kumshinda Mujinga Frazier wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kwa pointi 5-0 katika uzito wa Light ukumbi wa Bukom Arena Jijini Accra.

Kwa ushindi huo, Ezra Paul Mwanjwango amejihakikishia Medali ambayo inakuwa ya pili kwa timu ya taifa ya Tanzania ya Ndondi za Ridhaa ‘Faru Weusi wa Ngorongoro’ baada ya Mussa Maregesi wa uzito wa Cruiser.

Katika Nusu Fainali, Ezra Paul Mwanjwango atakutana na Andrew Chilata wa Zambia na hata kama atapoteza tayari ana uhakika wa kupata Medali ya Shaba, ambayo hutolewa kwa wana Nusu Fainali wote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live