Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Tanzania kupeleka wawili mashindano ya Ndondi India

Tanzania Boxing Tanzania kupeleka wawili mashindano ya Ndondi India

Tue, 7 Mar 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Mabondia Rahma Joseph Maganga na Beatrice Ambros Nyambega kwa mara ya kwanza wataiwakilisha nchi kwenye mashindano ya dunia ya ngumi kwa wanawake nchini India.

Mashindano hayo yajulikanayo kama IBA women's Boxing, yataanza Machi 15-31 yakishirikisha mabondia wa uzani tofauti kutoka mataifa tofauti duniani.

Katibu mkuu wa Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT), Makore Mashaga amesema ni mashindano yanayohusisha nchi wanachama wa chama cha ngumi cha Dunia (IBA).

"Tayari mabondia wapo kambini, wanaendelea na mazoezi chini ya makocha, Samwel Batmani na Mohamed Abubakar.

Hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa mabondia hao kuiwakilisha nchi kwenye mashindano yadunia yanayoratibiwa na IBA, Chama kipya cha ngumi za ridhaa cha kimataifa.

Kwa mujibu wa Mashaga, timu hiyo ilipaswa kuwa na mabondia watatu, ingawa Halima Macho ameondolewa kutokana na ratiba zake nyingine za kazi.

Chanzo: Mwanaspoti