Kamati ya Utendaji ya Kamisheni ya kusimamia Ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC), imemteua Mwanasheria Rashida Jamaldin Hussein, kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Rufaa ya kamisheni hiyo.
Taarifa iliyotolewana Idara ya Habari na Masoko leo Alhamis (Aprili 25) imeeleza kuwa Kamati ya TPBRC imefanya uteuzi huo kupitia kikao chake cha 13/04/2024, kilichofanyika jijini Dar es salaam.
Mwanasheria Rashida ameteuliwa kuiongoza Kamati hiyo akitarajia kushirikiana na Wajumbe wanne, ambao wanaaminiwa watafanyakazi kwa weledi.
Wajumbe walioteuliwa kwenye Kamati hiyo ni Kulwa Makalanga, Sadah S. Kasonso, Edward Emmanuel Lykwipa na Iddi Bilali Toatoa.