Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

TPBRC yafuta matokeo ya April 22

A236B964 354B 4258 A9EE 4EAC378B26F0.png TPBRC yafuta matokeo ya April 22

Thu, 27 Apr 2023 Chanzo: Dar24

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini Tanzania ‘TPBRC’ imefuta matokeoya pambano la Loren Japhet dhidi ya Juma Choki lililofanyika Jumamosi (April 22) katika ukumbi wa Tanzanite, Morogoro.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu Mkuu wa TPBRC imeeleza kuwa matokeo ya pambano hilo ambalo lilimalizika kwa Juma Choki kutangazwa mshindi kwa Point.

Maamuzi ya kutengua ushindi wa Bondia huyo yamekuja baada ya kamati ya muda ya TPBRC inayoundwa na Rais wa Kamisheni ambayo wajumbe wake ni Nassoro Chuma, Haji Ngoswe, Edward Emmanuel Lyakwipa, Agapito Basil, Salum Mgeni na Chaurembo Palasa kwa ajili ya kupitia upya video na kujiridhisha kulikuwa na mapungufu.

Pambano hilo liliamuliwa kwa ushindi wa point (Majority Decision) kwa Juma Choki kwa matokeo yaliyotolewa na Majaji (i) George Sabuni 77/75, (ii) Omari Yazidu 75/77 na (iii) Mohamed Mganza 74/78. Baada ya Kamati kupitia upya video ya pambano hilo, imeyafuta matokeo hayo na kutoa uamuzi kuwa ni Droo.

Hata hivyo TPBRC imefikia maamuzi ya kuwaita majaji wa pambano hilo kwa hatua zaidi ambao ni . Kamati ya Muda ya TPBRC pia imefanya maamuzi ya kulifuta pambano la Abdallah Yoba dhidi ya George Odongo.

Pambano hilo limefutwa kutokana na kutokidhi masharti ya mkataba ambapo awali bondia Abdallah Yoba alisaini mkataba wa pambano la mizunguko 6 dhidi ya bondia Jitu Rajabu na siku ya kupima uzito, muandaaji alimbadilishia mpinzani na kumuweka Goerge Odongo tofauti na Jitu Rajabu aliyetajwa kwenye mkataba na siku ya pambano muandaaji alipunguza mizunguko kutoka 6 hadi minne kinyume na mkataba.

Pambano kati ya Leonard Dedan vs Babuu Luda, nalo limefutwa na Kamishna wa pambano Nassoro Chuma kutokana na wasaidizi wa ulingoni wa kambi zote mbili za mabondia hao kusababisha vurugu ulingoni. Wahusika wa kambi zote mbili wameitwa kwenye Kamati ya Nidhamu, Utatuzi na Usuluhishi wa Migogoro kwa hatua zaidi.

Chanzo: Dar24