Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Serikali yatia mkono adhabu ya Mwakinyo TPBRC

Damas Ndumbaro Ngumi Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: Dar24

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo imesema kuna haja ya kufuatilia mwenendo wa mashtaka ili kubaini uhalali wa adhabu iliyotolewa na Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBRC) ya kumfungia bondia Hassan Mwakinyo.

Hayo yamebainishwa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Damas Ndumbaro wakati akizungumza na waandishi wa habari nje ya ofisi za Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) jijini Dar es salaam.

“Sisi kama wizara tutakaa na BMT (Baraza la Michezo la Taifa), lakini tutakaa pia na TPBRC, ili kuweza kupata taarifa rasmi ya nini kimetokea na misingi ya hiyo adhabu, baada ya kupata taarifa hiyo ndipo tutashauriana na wahusika wote namna adhabu hiyo ilivyotolewa, uhalali wake kama adhabu hiyo ni sahihi ataitumikia, kama kuna mushkeli kidogo tutakaa na kushauriana kuona tunafanyaje,” amesema Waziri huyo.

Jui Jumanne (Oktoba 10) TPBRC ilitangaza kumfungia Mwakinyo ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja na faini ya Sh milioni moja kwa kinachoelezwa Septemba 29 mwaka huu, bondia huyo aligomea kupanda ulingoni katika pambano lililofahamika ‘The Return of Champ’ huku pambano lake likiwa ndio kuu.

Chanzo: Dar24