Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Sababu ya nyota ya Muhammad Ali kuwekwa ukutani na sio chini

Hollywood Walk Of Fame Muhammad Ali

Mon, 15 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hollywood Walk of Fame ni nyota ya heshima ambayo hutunukiwa kwa watu mashuhuri ambao wanamchango katika tasnia ya burudani, kuna zaidi ya nyota 2500 ambazo wametunukiwa watu maarufu ikiwa ni pamoja na waigizaji, wanamuziki, watayarishaji, vikundi vya muziki na Tamthiliya.

Mwaka 2002 bondia Muhammad Ali naye alitunukiwa nyota yake, hakuwa Mwigizaji ila ni kutokana na uwezo wake wa ndondi akipigana uzito wa juu (Heavy Weight) na kutajwa kama bondia wa uzito wa juu wa muda wote.

Kwa kawaida "Hollywood Walk of Fame" huwekwa chini lakini kwa Muhammad Ali yake ipo ukutani, Wakati alipopewa nyota hiyo mwaka wa 2002 akiwa na umri wa miaka 59 wakati huo alisema kwamba hakutaka jina lake likanyagwe na watu wasio mheshimu.

"Nimebeba jina la Mtume Muhammad, na haiwezekani kwamba niruhusu watu kukanyaga jina lake," alisema Ali.

June 4,2016 Muhammad Ali alifariki Dunia akiwa na umri wa miaka 74 akitibiwa hospitalini mjini Phoenix katika jimbo la Arizona, Marekani. Ali anasalia kuwa bingwa wa uzito wa juu kuwahi kutokea na wa muda wote Duniani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live