Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roma Mkatoliki: Msimsimange nwanetu Mandonga

Ndonga Bou Mandonga

Sun, 31 Jul 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kufuatia Pambano la Bondia Karim Mandonga usiku wa kuamkia leo, kupigwa kwa TKO Round ya 4 dhidi ya mpinzani wake Bondia Shaban Kaoneka, rappa Roma ambaye ni shabiki wa Mandonga ameeleza haya machache kuhusiana na Mandonga kupoteza pambano lake.

Roma ameeleza Mandonga asisimangwe, bado ana Imani nae, akitolea mfano wa pambano la Bondia mkongwe Mike Tyson na Buster Douglas, katika pambano la mwaka 1990.

"Tarehe 11, February Mwaka 1990, #BusterDouglas alimpiga K.O #Tyson na Mike akashindwa kuendelea na pambano!! Suala la kupigwa kwenye mchezo wa #Vitasa ni la kawaida sana. So msimsimange mwanetu #Ndonga “BADO NINA IMANI NA YEYE” amesema Roma kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Fahamu, hili ni pambano la pili mfululizo kwa Bondia Karim Mandonga kupoteza kwa TKO.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live