Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Roja Mjeshi afariki dunia, kuzikwa leo saa 10 jioni

Bondia Sds Roja Mjeshi afariki dunia, kuzikwa leo saa 10 jioni

Thu, 25 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Rajab Hawaji 'Roja Mjeshi' aliyefariki dunia usiku wa kuamkia leo na anatarajiwa kuzikwa leo jioni.

Familia ya marehemu, imesema kuwa, mwili wa bondia huyo unatarajiwa kuhifadhiwa saa 10:00 jioni nyumba ya hospitali ya Tandale, jijini Dar es Salaam.

Kaka wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina la Mwinyi Bila, naye ni bondia na mwamuzi wa mchezo huo, amesema ndugu yake alikuwa anasumbuliwa kwa muda mrefu, lakini alikuwa anajikaza kwani hakuwa mtu wa kupenda kulala.

Bila amesema awali aliwahi kufanyiwa upasuaji, lakini hali yake ilibadilika ghafla jana na kulazimika kumuwahisha hospitali ya Mwananyamala na baada ya vipimo wakagundua utumbo umetoboka.

"Alikuwa anaumwa kwa muda mrefu na aliwahi kufanyiwa upasuaji, hivyo kifo chake hakihusiani na mchezo wa ngumi," amesema.

Mwenyekiti wa Chama cha Mabondia wa Kulipwa Tanzania (TPBA), Japhet Kaseba amesema wanasikitishwa kumpoteza bondia huyo na kuwaomba wana michezo kujitokeza kumzika mwenzao.

"Kwa wale wanaotaka kuja msibani, wakifika Tandale Hospital ni rahisi kufika nyumbani, Mjeshi ni maarufu sana maeneo haya," amesema.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live