Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rekodi 10 matata kwenye ulingo wa masumbwi

Man Pacquiao Vs Myweather Rekodi 10 matata kwenye ulingo wa masumbwi

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mchezo wa masumbwi umeshirikisha mabondia wa maana kwelikweli ambao wameondoka na kuacha alama zao.

Kuna mabondia hao, mavitu yao ya ulingoni yaliwafanya wajitofautishe na wengine kwa nyakati walizokuwa wakipigana na kuandika hostoria kwenye mchezo huo wa masumbwi.

Makala haya yanahusu rekodi matata kabisa zilizowahi kutokea kwenye mchezo wa masumbwi na kubaki kwenye kumbukumbu za vitabu vya kihistoria vya mchezo huo.

Unajua ni mabondia gani waliweka rekodi hizo zinazodumu kwenye mchezo huo wa kupigana ngumu ulingoni?

1) Bondia aliyestaafu bila ya kupigwa: Floyd Mayweather

Floyd Mayweather si bondia wa kwanza kustaafu bila ya kupigwa kwenye pambano lolote lile, lakini alikuwa wa aina yake kwenye kuwahi kutokea wakati anapigana. Mayweather aliwachapa mabondia kibao walikuwa mabingwa wanaoshikilia mikanda ya ubingwa wa dunia kuliko bondia yeyote yule, na alishinda mapambano 23 ya aina hiyo wakati anapigana.

Karibu nusu ya kipindi chake alichokuwa bondia, alikuwa akipigana na mabondia mahiri ulingoni. Lakini, hadi anastaafu, alikuwa na rekodi ya 50-0, kwa maana hajapoteza pambano lolote.

Mayweather alishinda pia mataji matano ya ubingwa wa madaraja tofauti katika kipindi chote, huku mpinzani wake mkubwa Mayweather ni Manny Pacquiao, ambaye anashika namba mbili kwa kushinda mara nyingi mapambano dhidi ya mabingwa, 22.

2) Mataji mengi kwenye uzito tofauti: Manny Pacquiao

Kuna sababu kwa nini Manny Pacquaio na Floyd Mayweather yalikuwa majina makubwa kwenye mchezo wa masumbwi katika kipindi cha miongo miwili iliyopita.

Pacquaio alikuwa na uzito wa 111 lbs wakati anashinda ubingwa wake wa kwanza wa dunia na alibadili uzito kwa jumla ya 38 lbs katika maisha yake ya masumbwi na kushinda ubingwa katika kila uzito.

Jambo hilo lilimfanya kuwa bondia mshindani kwelikweli na kupambana na mabondia walikuwa mahiri ulingoni na kuwashinda. Kuonyesha ubora wa bondia huyo, wakati anapigana na Mayweather alikuwa na uzito wa 130 lbs kwenye pambano lao la kwanza, hivyo Pacman, alilazimika kutengeneza uzito wake ili uwe sawa na pambano hilo lilipigwa.

3) Kushinda mikanda mingi ya kibingwa: Muhammad Ali

Ali kiwango chake cha ulingoni kilikuwa matata kwelikweli. Hakika, alikuwa mfalme wa ulingo kwa kuwa alishinda mapambano mengi ya kibingwa kuliko bondia yeyote yule.

Na hilo ndilo lililomfanya kuwa maarufu katika dunia hiyo ya masumbwi. Alikuwa kama anatoa burudani ulingoni, lakini mwisho wa pambano aliibuka mshindi.

Kwa kifupi tu, alishinda ubingwa wa mikanda yote mikubwa na kuandika historia ya kuwa bondia bora zaidi kuwahi kutokea kwenye mchezo wa masumbwi. Ali alishinda mikanda hiyo wakati alipowatwanga Sony Liston, George Foreman na Leon Spinks.

4) Kutopoteza pambano muda mrefu: Packey McFarland

Kama ulivutiwa na rekodi za Mayweather, basi subiri kumfahamu bondia ambaye anashikilia rekodi mara mbili ya hizo zinazoshikwa na Floyd. McFarland alikuwa bondia na kupambana mwishoni mwa karne ya 19 na mapema karne ya 20, ambapo rekodi zake zinanyesha kwamba alipigana mapambano 70 na hajapoteza hata mara moja kabla ya kustaafu.

Kuweka rekodi yake kuwa tamu zaidi, kwenye pambano hayo, alishinda mara 50 kwa knockout. Na kipindi hicho anapigana, McFarland masumbwi pia yalikuwa yanahitaji mabadiliko makubwa sana.

5) Kushinda Knockout mara nyingi: Billy Bird

Billy Bird alionekana kuwa ni mtu wa kawaida sana kuliko kutambulika kwa ubora wake kwenye ulingo wa masumbwi.

Lakini, mtu huyo aliyekuwa anaonekana kuwa wa kawaida, ndiye anayeshikilia rekodi ya kushinda mara nyingi mapambano yake ya KO na ameshinda 139.

Kwa jumla wake, Billy Bird alikuwa mwamba, alipigana mapambano 356 katika maisha yake ya masumbwi mwanzoni mwa karne ya 20. Bondia, Archie Moore, ndiye aliyekuwa anamkaribia Billy kwa kushinda mara nyingi kwa KO, mara 132, ambaye pia alikuwa anapigana mwanzoni mwa karne ya 20. Kwa mabondi waliopo kwa sasa, anashikilia rekodi ya kushinda knockout nyingi ni Deontay Wilder, mara 42.

6) Bingwa wa dunia mwenye umri mkubwa: Benard Hopkins

Hopkins alibadili mipango ya kustaafu ya mabondia wengi sana wakati alipomchapa Jean Pascal na kushinda mkanda wa WBC, wakati huo alipokuwa na umri wa miaka 46.

Hiyo ilionyesha namna bondia huyo alivyokuwa amejituza vyema baada ya kustaafu na kurudi ulingoni na kushinda pambano.

Hopkins alikuwa bondia tishio sana kipindi chake, lakini ile staili yake ya kujilinda ilionekana kuwa tatizo. Katika dunia ya masumbwi, mabondia wengi wanaonekana kustaafu wakiwa na miaka 40 na hilo lilichagizwa zaidi na Hopkins baada ya kushinda ubingwa wa dunia akiwa bondia mwenye umri mkubwa, miaka 46.

7) Bondia mfupi kushinda ubingwa: Tommy Burns

Urefu wa futi 6 kwenye masumbwi kunatajwa kuwa ni mfupi, hasa baada ya mabondia wengi waliokuwa wakionekana kuwa mahiri ulingoni kama Tyson Fury na Deontay Wilder walikuwa na vimo vya futi 7 na futi 6 na inchi 7 mtawalia.

Lakini, kimo cha Burns kilikuwa futi 5 na inchi 7, lakini alishinda ubingwa wa dunia wa uzito wa juu. Na kinachonogesha zaidi, Burns alikuwa bondia pekee mzaliwa wa Canada kupigana kwenye uzito wa juu ya kushinda ubingwa kwenye historia ya taifa hilo.

Kingine alichokionyesha Burns ni udogo wa umbo hauwezi kuwa tatizo baada ya kufanikiwa pia kutetea mkanda wake huo wa ubingwa mara 13.

8) Mapambano mengi na kushinda: Len Wickwar

Hutakiwi kuwa mtunza historia wa masumbwi kufahamu hilo lilitokea mwanzoni mwa kipindi cha mapambano ya mawumbwi na mabondia walikuwa wakipigana zaidi ya mara mbili ndani ya mwezi mmoja.

Wickwar alipambana mwanzoni mwa karne ya 20 na alistaafu akiwa na rekodi ya 342-86-43.

Bondia huyo alishinda mapambano 94 na kinachovutia, yote alishindwa kwa knockout. Rekodi yake ya kushinda pambano mengi na kushinda haijavunjwa kwa miaka ya karibuni hasa kwa kipindi hiki ambacho masumbwi yamekuwa na mabadiliko makubwa, mabondia hawapigani mara kwa mara.

9) Likizo ndefu baina ya ubingwa wa dunia: George Foreman

George Foreman alishinda ubingwa wake wa kwanza wa uzito wa juu mwaka 1973 na alistaafu masumbwi 1977.

Alikuwa likizo kwa muda mrefu kwenye masumbwi kabla ya kurejea tena ulingoni na kushinda kwa knockout dhidi ya Michael Moore na kushinda ubingwa wa mkataba wa WBA na IBF akiwa na umri wa miaka 45 na ilikuwa tofauti ya miaka 21 kati ya ubingwa wa kwanza wa dunia na uliofuatia.

10) Bingwa wa uzito wa juu aliyestaafu bila kupigwa: Rocky Marciano

Kustaafu masumbwi bila ya kupoteza akiwa bingwa wa dunia ni kitu bora na kikubwa kwa bondia yeyote duniani, lakini kinachovutia zaidi ni kuwa bingwa wa uzito wa juu.

Bondia Rocky Marciano alikuwa matata kwelikweli ulingoni, ngumi zake zilikuwa matata. Pengine, Tyson Fury anaweza kupita kwenye nyayo hizo kama atashinda ubingwa wa dunia kwenye uzito wa juu kisha akastaafu.

Rekodi ya sasa ya Fury ni 31-0-1, wakati Marciano alistaafu masumbwi akiwa na rekodi ya 49-0.

Chanzo: Mwanaspoti