Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rasmi: Kell Brook astaafu ngumi

Kell Brook Bn.jpeg Kell Brook

Mon, 9 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bingwa wa zamani wa dunia uzani wa Welterweight Muingereza Kell Brook, ametangaza kustaafu rasmi ngumi akiwa na rekodi ya kushinda mapambano 40 kati ya 43 katika ngumi za kulipwa.

Kell mwenye umri wa miaka 36, Pambano lake la mwisho lilikuwa la ushindi wa raundi ya sita, dhidi ya muingereza mwenzake Amir Khan, Februari mwaka huu.

Kell alishikilia ubingwa wa Dunia wa IBF kutoka mwaka 2014 hadi 2017 baada ya kumtwanga Shawn Porter kwa pointi, alipoteza ubingwa huo baada ya kuchapwa kwa KO na Errol Spence Jr (2017).

Alianza ngumi za kulipwa mwaka 2004 akiwa na umri wa miaka 18, baada ya kucheza ngumi za ridhaa kwa miaka 6.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live