Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa ngumi za kulipwa Tanzania yamemkuta

Ngumi Pic Rais wa ngumi za kulipwa Tanzania yamemkuta

Fri, 22 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBRC) imemuita kwenye kamati ya Nidhamu, utatuzi na usuluhishi wa migogoro, rais wa kampuni ya ngumi za kulipwa ya PSTR, Emmanuel Mlundwa kujibu tuhuma za kutumia nyaraka za chama hicho tofauti.

Hata hivyo Mlundwa amesema kesi hiyo ni ndogo kwake, atakwenda kuisikiliza kamati na anavielelezo vyote vya kufanya majukumu anayotuhumiwa na TPBRC.

Rais wa TPBRC, Chaurembo Palasa ameiambia Mwanaspoti kuwa, Mlundwa alituma baadhi ya nyaraka za ngumi kwa wamiliki wa mtandao wa rekodi za mabondia wa dunia (Boxrec) bila kuwakopi viongozi wa TPBRC ambao ndiyo wasimamizi wa ngumi za kulipwa nchini.

"Lakini pia katika nyaraka hiyo alimtaja makamu wa rais (Agapeter Basil 'Mnazareth') kuwa ndiye rais wa TPBRC, akazituma Boxrec kisirisiri jambo ambalo ni kosa," amesema Palasa.

Amesema wamemuita kwenye kamati Mlundwa ili kueleza kwa kina lengo la kuandika barua Boxrec yenye maudhui yanayohusisha TPBRC kwa kupitia anawani ya kamisheni kisirisiri," amesema Palasa akifafanua kwamba taarifa hiyo ilikuwa inahusu baadhi ya mikanda ya ubingwa.

"Kamati ilimuita Julai 18 hakutokea, Julai 22 (kesho) imemuita tena kumsikiliza," alisema huku Mlundwa akisisitiza kwamba kesi hiyo ni ndogo kwake na atakwenda.

"Julai 18 niliwajibu kwa email 'barua pepe' na kopi nikaituma BMT ambao ndiyo walini-point mimi kutuma taarifa za mabondia Boxrec," amesema.

Amesema yeye kama katibu wa chama cha waamuzi wa ngumi za kulipwa Tanzania, alitaka tuhuma zote zinazomkabiri zipelekwe Baraza la Michezo.

"Niliwajibu TPBRC kwa email, hard copy walikataa kuipokea, lakini kopi nilizipeleka BMT na kesho nitakwenda kwenye kamati na nyaraka zangu, lakini niseme tu, hiyo ni kesi ndogo sana kwangu," amesema Mlundwa.

Chanzo: Mwanaspoti