Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais alifuta Pambano la Mandonga

Screenshot 20220925 005151 Mandonga Karim Mandonga

Sat, 24 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania (TPBRC) Chaurembo Palasa ametangaza kulifuta pambano la raundi nne kati ya Bondia Karim Mandonga dhidi ya Salim Abeid kutokana na Mwamuzi wa pambano hilo kutotenda haki kwa kuchezesha chini ya kiwango.

Pambano hilo la Super Middle Weight lililokuwa la raundi 4, limefutwa baada ya mwamuzi kufanya maamuzi yasiyo sahihi mara kadhaa wakati wa pambano hilo na kutafsirika amekiuka taratibu za mchezo.

Mandonga alimsukuma mpinzani akaanguka chini na refarii akamuhesabia kana kwamba Mandonga amemuangusha kihalali mpinzani.

Karima Mandonga alisukumiwa makonde yaliyompeleka chini na refarii hakumuhesabia jambo ambalo si sahihi na kupelekea Rais wa Shirikisho la ngumi nchini Chaurembo Palasa kulifuta pambano hilo licha ya kumalizika kwa raundi nne.

"Watu wote tumeona pambano lilivyokwenda, kwa mamlaka niliyo nayo pambano hili nimelifuta kwa sababu refa hakufanya haki, kwa hiyo pambano nimelifuta na halina mshindi," amesema Chaurembo.

Pambano hilo ambalo ni la saba kwa mandonga tangu aanze kucheza ngumi za kulipwa, lilikuwa la utangulizi katika pambano kati ya Mtanzania Twaha Kiduku na Abdo Khaled,raia wa Misri, wanaowania mkanda wa UBO Intercontinental.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live