Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pulev, Class watikisa, mataji yabaki Bongo

Ndondi Pic Data Pulev, Class watikisa, mataji yabaki Bongo

Wed, 3 Feb 2021 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Imani MakongoroMore by this Author REKODI imewekwa. Ndio, bondia Ibrahim Class na Kubrat Pulev wameweka rekodi katika pambano la The Rumble in Dar lililopigwa usiku wa kuamkia jana, huku mikanda ya ubingwa wa WBF wa Mabara na International ikibaki nchini.

Mtanzania huyo na Pulev, raia wa Bulgaria walikonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza Ukumbi wa Next Door Arena, Masaki jijini Dar es Salaam kwa namna walivyoumudu ulingo. Akicheza nyumbani, Class alionyesha ukomavu, nidhamu na ubora vilivyomsaidia kuongoza raundi zote 12 na kutangazwa bingwa mpya wa Mabara wa WBF kwa pointi za majaji wote dhidi ya Dennis Mwale wa Malawi.

Majaji Ibrahim Kamwe, Kulwa Makaranga na Abdallah Neneko walitoa pointi 116-114, 118-110 na 117-111 kwa Class katika pambano hilo lililochezeshwa na refa wa kike, Pendo Njau na kusimamiwa na Rais wa WBF, Goldberg Howard. “Hakuanza vizuri raundi ya kwanza, ilipokwisha tu nilimwambia sitaki umkimbie mpinzani wako, weka guard kujilinda na simama upigane,” alisema Kocha Habibu Kinyogoli muda mfupi baada ya pambano.

Kocha huyo anayemnoa Class muda mrefu, alisema japo alikuwa na wasiwasi kutokana na bondia wake kucheza akiwa ametoka kwenye dozi ya malaria, lakini alipigana kwa maelekezo na kuongoza raundi zote.

Akizungumzia ushindi wake, Class alisema ulikuwa wa jasho na damu, kwani mpinzani wake hakuwa bondia wa kitoto.

“Nilianza kumsoma raundi ya kwanza, Mwale hachoki, harudi nyuma na muda wote ana uchu wa kushambulia, ila uzoefu, mazoezi na maelekezo ya kona yangu baada ya kuisha raundi ya kwanza vilinisaidia.”

Chanzo: mwanaspoti.co.tz