Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Promota: Maandalizi yanakwenda vizuri sana

Class Pic Data Promota: Maandalizi yanakwenda vizuri sana

Mon, 15 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Promota wa Pambano la Usiku wa Class, Mndeme Sports Promotion, amefichua kuwa, kutokana na maandalizi mazito yanayofanywa na mabondia, Ibrahim Class na Said Chino, anaamini watapasuana kweli.

Class na Chino wanatarajia kupanda ulingoni Mei 27, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Warehouse uliopo Masaki jijini Dar ambapo pia Cosmas Cheka atazichapa na Issa Nampepeche, Haidary Mchanjo vs Yohana Mchanja, Emanuel Mwakyembe vs Allan Kamote, Alex Kachelewa vs Nicolas Mdoe, Halima Vunjabei vs Flora Machela na Eugine Kayange vs Halima Bandora.

Promota wa pambano hilo, Esther Mndeme, amesema maandalizi ya pambano hilo yanaendelea vizuri na anawashukuru wadhamini waliojitokeza kwa kumpa sapoti katika pambano hilo.

“Kwanza niwashukuru wadhamini wangu, kwa kujitoa kusapoti hili pambano ambalo Ibrahim Class na Said Chino watacheza pambano kuu, hili ni jambo kubwa la kupongeza ingawa bado milango ipo wazi kwa upande wa udhamini.

“Lakini upande wa maandalizi ya tunashukuru yanaendelea vizuri kwa mabondia wote akiwemo Idd Pialali ambaye atacheza na Simon Ngoma wa Zambia, Ibrahim Class ameweka kambi hapahapa ingawa mpinzani wake Said Chino ameweka kambi Morogoro,” amesema Mndeme.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live