Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pius Mpenda ashinda kwa TKO Dubai

Mpenda Pius Pius Mpenda ashinda kwa TKO Dubai

Mon, 22 May 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia namba moja wa uzito wa kati hapa nchini, Pius Mpenda kutoka Kambi maarufu ya ngumi ya Naccoz, Mabibo jijini Dar es salaam, amefanikiwa kuibuka na ushindi wa Technical Knock Out (TKO) raundi ya 8 dhidi ya mpinzani wake Moughit El Moutaouakil kutoka nchini Morocco.

Pambano hilo lisilo la ubingwa, limepigwa usiku wa kuamkia jana Jumapili mjini Dubai, umoja wa falme za kiarabu (UAE), ambalo linakuwa pambano la pili kwa Mpenda kushinda nje ya Tanzania, baada ya Desemba 2022 kumchapa Farouk Daku na kushinda ubingwa wa WBU nchini Uganda.

Katika pambano hilo lililoandaliwa na Promota Eisa Al Dah, Mpenda aliongozana na mabondia wengine wawili wa Tanzania, ambao ni Mwinyi Mzengela aliyepoteza kwa Knock Out (KO) na Sarafina Bela aliyepoteza kwa pointi.

Kwa ushindi huo, Mpenda anakuwa na rekodi ya kucheza mapambano 7 akishinda 6 na kupoteza 1 pekee.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live