Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano la Mwakinyo lina mengi nyuma ya Pazia, Promota azungumza hili..!

Mwakinyo Gloves .jpeg Bondia Hassan Mwakinyo

Sun, 9 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

April 23 ngumi zitapigwa sana tu jijini Dodoma wakati bondia maarufu nchini, Hassan Mwakinyo atakapopanda ulingoni kuzipiga na Kuvesa Katembo wa Afrika Kusini, lakini pambano hilo likisaidia kuwanufaisha mabinti waliolamba dili ya Sh 35 Milioni.

Lengo la pambano hilo ni kusaidia kupata pesa za kununua taulo za watoto wa kike inatakiwa idadi ya 40,000 zitakazogawiwa kwa wanafunzi wa mikoa wa nyanda za juu Kusini na kabla ya mabondia hao kupanda ulingoni, tayari kampuni ya Softcare Sanitary Pads imetoa taulo 20,000 na fedha ambavyo kwa pamoja vina thamani ya Sh. 35 Milioni, ili kuunga mkono juhudi hizo kwa wanafunzi wa vijijini.

Promota wa shindano hilo, Sophia Mwakagenda, aliye pia Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mbeya, alisema katika kuona umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike waliamua kuandaa pambano hilo ili kuchangia taulo za kike ili ziweze kuwasaidia kuondoa vikwazo kwenye masomo yao.

Promota huyo alitaja sababu kuchagua pambano hilo kufanyika Aprili 23, Dodoma ni katikati ya nchi, pia kushirikiana na wabunge ambao ni rahisi kuwapata kipindi hiki ambacho bunge linaendelea.

Kwa upande wa Mkurugenzi Mkuu wa Dorrycare Technology Company, Victor Zang alisema lengo la pambano hilo ni kuchangisha fedha za kununua angalau taulo za kike 40,000 na kuzipeleka kwenye jamii hususani kwa wanafunzi na wanawake wenye mahitaji maalumu ili kuwahakikishia hedhi salama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live