Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano la Fury vs Usyk laingia doa

Usyk Vs Tyson Fury Pambano la Fury vs Usyk laingia doa

Mon, 5 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Pambano lililokuwa likisubiriwa kwa hamu kati ya Tyson Fury na Oleksandr Usyk lililopangwa kufanyika tarehe 17 February mwaka huu huenda lisifanyike tena hiyo ni baada ya Fury kupata jeraha kubwa usoni la kupasuka akiwa kwenye mazoezi yake huko Saudia Arabia ya kujiandaa na pambano hilo.

Uongozi wa Fury umetoa taarifa rasmi ya jeraha hilo alilopata bondia wao na sasa wanachongojea ni majibu kutoka kwa daktari kwamba jeraha hilo litachukua muda gani hadi kupona. Nae Fury amewaomba radhi waandaaji wa pambano, mashabiki na mpinzani wake Usyk kwa kutokupigana kwenye tarehe waliyopanga hapo awali.

Dunia inangojea kujua ni tarehe ngapi pambano hilo litapangiwa ili wapate kushuhudia utamu wa ndondi hizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live