Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano la Fury, Usyk kuweka rekodi hii

Usyk Vs Tyson Fury Pambano la Fury, Usyk kuweka rekodi hii

Fri, 24 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Tyson Fury atakapocheza dhidi ya Oleksandr Usyk Februari 17 mwakani nchini Saudi Arabia ataweka rekodi ya kuwa bondia wa uzito wa juu anayelipwa pesa ndefu kwenye pambano moja katika historia ya mchezo wa masumbwi dunaini.

Promota wa bondia huyo aitwae Bom Arum amesema kuwa Fury atavuna kiasi cha pesa kinachokadiriwa Pauni Milioni 100 (Tsh.Bilioni 313.8) Kwa pambano lake dhidi ya Oleksandr Usyk, na hivyo atavunja rekodi ya malipo kwenye uzito wa juu (pambano rasmi).

Pambano la 'The Bite Fight' la Juni mwaka 1997 pambano la marudiano la Mike Tyson na Evander Holyfield, lilimfanya Tyson aweke rekodi ya kulipwa mkwanja mrefu kwenye uzito wa juu alipolipwa Dola milioni 30 (Tsh. Bilioni 75).

Chanzo: www.tanzaniaweb.live