Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano la Fury, Usyk kusogezwa mbele

Usyk Vs Fury Fight Pambano la Fury, Usyk kusogezwa mbele

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Frank Warren ambaye ni mwendeshaji wa michezo amesema kuwa pambano la Uzito wa juu kati ya Bondia Tyson Fury kutoka Uingereza dhidi ya Oleksandr Usyk kutoka Ukraine la kuwania Mikanda ya WBA, WBC, IBF & WBO (UNDISPUTED CHAMPIONSHIP) linatajwa kwamba halitofanyika tena Desemba 23 kama lilivyopangwa hapo awali na badala yake litapigwa Mwezi Februari Mwakani huko nchini Saudi Arabia

"Tulipanga kulifanya tarehe 23 Desemba. Sasa nadhani hilo haliwezekani. Tyson hawezi kuingia kambini baada ya pambano gumu kama hilo. Hizo ni wiki nane mbele. Anahitaji angalau muda kidogo kujipata yeye mwenyewe, mwili wake, arudishe hali ya kawaida. Kisha ajiandae kwa kambi. Pambano litakuwa mwanzoni mwa mwaka ujao." amesema Warren akiongea kwenye podcast ya masumbwi ya 5 Live

Fury alimshinda Francis Ngannou kwa utata mwingi sana Jumamosi kupitia uamuzi wa kuamuliwa kwa alama za Majaji huko nchini Saudi Arabia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live