Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pambano halipo! Tyson Fury amuita Anthony Joshua 'muoga na mjinga'

Joshuafury Copy Tyson Fury na Anthony Joshua

Tue, 27 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia maarufu Duniani, Tyson Fury ametamka kuwa amefuta mpango wa kupigana na Anthony Joshua huku akimtaja mpinzani wake huyo kuwa ni muoga kutokana na kutokuwa na msimamo wa kutoa majibu kuhusu kusaini mkataba wa pambano lao.

Fury alimpa muda Joshua kusaini mkataba huo hadi kufikia Septemba 26, 2022 ili pambano lao lifanyike Desemba 3, 2022, hivyo baada ya muda huo kupita bingwa huyo wa uzito wa juu Mkanda wa WBC, amesema atatafuta mpinzani mwingine.

“Sahau kuhusu poambano hilo… Imeisha hiyo, hakuna mkataba uliosainiwa mpaka sasa. Rasmi haipo tena, Joshua yupo kimya ni baridi… Sio mpiganaji huyo ni mtunisha misuli, hana uwezo wa kupigana na mimi. Nakutakia maisha mema na mwisho mwema!"

Tyson Fury amesema hayo baada ya mabondia wawili hao kushindwa kukutana jana kwa ajili ya kusaini mkataba wa pambano hilo.

Tyson Fury amemtaja Anthony Joshua kama “muoga” na “mjinga” ambaye uwezo wake wa ngumi kidunia umeporomoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live