Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Palasa Chaurembo apeta TPBRC

Chaurembo Palasa.png Chaurembo Palasa

Mon, 15 May 2023 Chanzo: Dar24

Baraza la Michezo la Taifa (BMT), limemwidhinisha bondia wa zamani wa mchezo wa ngumi za kulipwa nchini, Chaurembo Palasa, kuwa Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa ‘TPBRC’ baada ya kuibuka mshindi kwa kupata kura 19 dhidi ya mpinzani wake wa karibu, Meja Bakari Songoro aliyepata kura 15 huku kukiwa hakuna kura iliyoharibika kati ya 34 zilizopigwa.

BMT kupitia Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Allen Alex, Palasa alikuwa akitetea nafasi yake ya urais aliyoshinda mwaka jana baada ya kumbwaga Meja Bakari Songoro kwa kura moja.

Katika nafasi ya Makamu wa Rais wa Kamisheni hiyo, Nassoro Chuma, alikuwa mgombea pekee na amepita kwa kura 28 huku sita pekee zikiwa za hapana kwa upande wake.

Kwa upande wa nafasi ya Katibu Mkuu, George Silas, amembwaga kwa kishindo Ibrahim Kamwe ‘Big Right’ kwa kupata jumla ya kura 25 huku mpinzani wake huyo akiambulia kura nane pekee.

Nafasi ya mweka hazina ilikuwa na mgombea mmoja pekee, Elius Mlundwa, ambaye amepita kwa jumla ya kura 31 huku kukiwa na kura moja tu ya hapana.

Kwa upande wa nafasi nne za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji wa Kamisheni hiyo, daktari wa mchezo huo na Mjumbe wa Kamati ya Afya, Dk. Hadija Hamisi, ameshinda kwa kura 33 akifuatiwa na Abdallah Juma aliyepata kura 30 wakati Peter Kulunge akiwa amepata jumla ya kura 28 na Hamis Kimanga akiwa mjumbe wa mwisho katika wajumbe wa nne waliochaguliwa kwa kupata kura 24.

Baada ya ushindi huo, Palasa amewashukuru wajumbe wa mkutano mkuu kwa kumwamini na kumchagua kwa kipindi cha miaka minne kwa ajili ya kuongoza kamisheni hiyo huku akisema kuwa atahakikisha anaendeleza mipango mizuri ya kusimamia mchezo huo, akifuata maagizo yote yaliotolewa na serikali katika kuusimamia mchezo huo.

“Kwanza nataka niwashukuru wajumbe wote kwa kuweza kunipa ridhaa ya kunichagua kuongoza kamisheni yetu kwa kipindi cha miaka minne, niwakati wa kuvunja makundi yote na kujenga au kurudisha umoja tuliokuwa nao ili tuweze kupiga hatua kubwa katika mchezo tunachangamoto zinapaswa wetu wa ngumi.

“Najua nyingi ambazo kufanyiwa kazi, lakini kwa kufuata maelekezo na maagizo ya serikali kupitia sera ya michezo, ni imani yangu umoja wetu utasaidia kutupeleka mbali katika mchezo wetu,” amesema Palasa.

Katibu Mkuu wa Kamisheni hiyo, George Silas, amesema: “Nashukuru kwa nafasi mliyoweza kunipa, hii inaonyesha imani kubwa juu yangu katika kuhakikisha ngumi zetu zinapiga hatua, lakini kuweza kulinda maslahi ya mabondia wetu.

“Nataka niwaambie kwamba nitafanya kazi yangu wakati wote kwa sababu mchezo wetu unahitaji muda mwingi wa kuweza kuwahudumia wadau lakini kufuata na kusikiliza yote yatakayokuwa yakielekezwa na serikali kupitia BMT,” amesema Silas

Chanzo: Dar24