Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Pacquiao apotezwa ulingoni, Terence Crawford kumbeba

Pacq Pic Data Pacquiao apotezwa ulingoni, Terence Crawford kumbeba

Thu, 1 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Kama litatiki basi ndilo litakuwa pambano la kumpa 'uhai' kwenye masumbwi bondia nguli wa uzani wa welter, Manny Pacquiao ambaye ameporomoka mara dufu kwenye viwango vya ndondi.

Pacquiao ambaye hayumo kwenye orodha ya mabondia bora 50 'top 50' ya dunia kwenye kila uzani 'pound for pound' yuko mbioni kuzichapa na Terence Crawford bondia namba tatu wa dunia aayetamba nyuma ya kinara Saul Alvarez anayepigania uzani wa super middle raia wa Mexico na Tyson Fury bondia heavy weight mzaliwa wa Uingereza.

Pambano la Pacquiao na Crawford liko kwenye majadiliano ambayo yakitiki litapigwa Juni huko Falme za Kiarabu.

Pambano hilo litakuwa gumu kwa pande zote mbili kutokana na 'nature' ya mabondia hao ambao wote wanatumia mkono wa kushoto 'southpaw'.

Crawford atataka kuendeleza rekodi yake ya kutopigwa katika mapambano 37 aliyopigana wakati Pacquiao kama atashinda bila shaka ushindi huo utakuwa wa mafanikio zaidi kwake kutokana na rekodi yake kutetereka.

Bondia huyo aliyekuwa namba 10 wa dunia kwenye pound for pound na namba moja kwenye uzani wake wa welter, hivi sasa hayupo kwenye 'top 50' kwenye pande zote.

Bondia huyo ambaye jina laker halisi ni Emmanuel Dapidran Pacquiao au Pac Man kama anavyopenda kujiita mzaliwa wa Philippines kwa sasa rekodi yake kwenye ngumi inaonyesha hayuko hai, hivyo pambano hilo la juni uenda likarejesha makali yake hasa akishinda.

Kabla ya kuporomoka, Pacquiao ambaye alianza rasmi kuzichapa kwenye ngumi za kulipwa mwaka 1995 ana histopria ya kupigana mapambano 71 na kushinda 62, sare mbili na amechapwa mara saba ikiwamo kipigo cha pointi dhidi ya Floyd Mayweather Jr.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz