Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

OBFT kuleta kocha kutoka Kenya

E7b3a5888930b8d98c6696db303f4302.jpeg OBFT kuleta kocha kutoka Kenya

Tue, 16 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

SHIRIKISHO la Ngumi za Wazi Tanzania (OBFT) limesema kuwa linatarajia kumleta kocha kutoka Kenya kwa ajili ya kuinoa timu ya taifa itakashiriki mashindano mbalimbali ya kimataifa, ikiwemo Michezo ya Olimpiki.

Katibu Mkuu wa OBFT, Wekelo Willilo alisema juzi jijini Dar es Salaam kuwa hivi karibuni wanatarajia kupata kocha kutoka Kenya mwenye nyota tatu kwa ajili ya kuinoa timu ya taifa itakayoshiriki Michezo ya Olimpiki.

Tanzania hadi sasa haina kocha mwenye hadhi ya nyota tatu na hivyo wale walio na timu ya taifa kwa sasa, hawaruhusiwi kuisimamia timu wakati ikishiriki Michezo ya Olimpiki.

Mwaka 2016 Michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro, Brazil, timu ya ndondi ya Tanzania ilikwenda bila kocha wa mchezo huo na kulazimika kuazima kocha wa Kenya aliyesimamia timu hiyo, hatua ambayo ilizua maswali mengi.

Willilo alisema kuwa kwa sasa timu ya taifa inaendelea na mazoezi kujiandaa na mashindano ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Tokyo 2020 itakayofanyika Japan kuanzia Julai mwaka huu.

Alisema kuwa timu hiyo ambayo inafanya mazoezi kwenye Uwanja wa Ndani wa Taifa, Dar es Salaam na kurudi nyumbani, ilianza mazoezi hayo hivi karibuni.

Chanzo: www.habarileo.co.tz