Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ni zamu ya Dullah Mbabe Vs Katompa

Dullah Mbabe Chimwemwe Ni zamu ya Dullah Mbabe Vs Katompa

Mon, 3 Jul 2023 Chanzo: Dar24

Kampuni ya Peak Time Media, imeweka wazi kuwa pambano la marudiano kati ya Mtanzania, Dullah Mbabe dhidi ya Tshimanga Katompa linatarajia kupigwa kwenye Uwanja wa Kinesi Julai 15, mwaka huu.

Ikumbukwe tayari Mbabe ana kumbukukumbu za kuchapwa kwa pointi na Katompa mwaka juzi (2021), katika pambano ambalo lilipigwa kwenye Ukumbi wa PTA Sabasaba, Dar.

Promota wa pambano hilo kutoka Peak Time Media, Meja Seleman Semunyu ameweka bayana kuwa tayari maandalizi ya pambano hilo yanaendelea kupamba moto kutokana na muda ambao umebakia kuelekea kwenye pambano hilo.

“Binafsi tunashukuru Mungu maandalizi yanaendelea vizuri kwa sababu tumeanza na kutafuta Ndondo Championi wa kitaa, ambao mabingwa wake wataungana na Dullah katika pambano la Mwana Kulitaka siyo Kinyonge ambalo litapigwa kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar, “amesema Meja Semunyu.

Chanzo: Dar24