Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngumi yapigia hesabu nafasi mbili Olimpiki

Ngumi Pic Data Ngumi yapigia hesabu nafasi mbili Olimpiki

Wed, 24 Mar 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Wakati ikisubiri msimamo wa Shirikisho la ngumi za kulipwa la dunia (AIBA), Shirikisho la Tanzania (BFT) inapigia hesabu ya kuwapeleka mabondia wawili kwenye michezo ya Olimpiki.

Zaidi ya wanamichezo 11,091 wanatarajiwa kushiriki kwenye Olimpiki wakichuana katika michezo 33 tofauti ikiwamo ngumi.

Awali kamati ya Olimpiki ya Kimataifa (IOC) ilieleza kuuondoa mchezo wa ngumi kwenye michezo ya Olimpiki kabla ya kuirejesha na kufanya mashindano maalumu ya Afrika mjini Dakar, Senegal kwa ajili ya kutafuta viwango vya Olimpiki.

Katika michezo hiyo ya Dakar, Michael Isendi na Yusuph Changalawe waliondoshwa kwenye robo fainali huku wengine wawili wakipigwa kwenye hatua za awali.

"Isendi na Changalawe ndiyo tunawapa nafasi ya kushiriki Olimpiki kama AIBA itabadili muundo wa mabondia katika nchi wanachama kufikia viwango vya Olimpiki," amesema katibu mkuu wa BFT, Lukelo Wililo.

Amesema kuna utaratibu ambao AIBA inaufanya ili mabondia wafuzu kushiriki Olimpiki kutokana na renki zao, hivyo mpango huo ukikamilika, kwa Tanzania ni Isendi na Changalawe ndiyo watakaopenya.

"Hawa wawili ndiyo wana renki nzuri kidunia, ni miongoni mwa mabondia 50 bora, hivyo mpango huo wa AIBA ukikamilika Tanzania tutawakilishwa na mabondia wawili kwenye Olimpiki ya msimu huu," anasema.

Anabainisha kwamba wakati wakaisubiri mpango huo, pia mabondia wa timu ya taifa wanaendelea na maandalizi wakijiandaa pia na mashindano ya dunia ya kufuzu ambayo yamepangwa kufanyika Mei mwaka huu nchini Ufaransa.

"Japo kuna uwezekano mashindano ya Ufaransa yakafutwa, lakini hatuwezi kuacha kujiandaa nayo hadi pale AIBA itakapotuba taarifa rasmi na mazoezi yetu yataendelea kwa ajili ya kuchuana sasa kwenye Olimpiki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz