Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ngumi jiwe! Bondia atapika ulingoni

Bondia Tapika.jpeg Ngumi jiwe! Bondia atapika ulingoni

Wed, 23 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bondia Hemed Rashid amepoteza pambano kwa TKO dhidi ya Iman Bariki ‘Man Chuga’ baada ya kushindwa kuendelea kutokana na kuumia.

Katika pambano hilo la Dar Boxing Derby kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es Salaam bondia huyo alikimbizwa Hospitali ya Mkoa wa Temeke kwa ajili ya matibabu zaidi.

Hemed alipoteza pambano raundi ya nane baada ya kupigwa ngumi mfululizo huku akionekana kuchoka kabla ya mwamuzi kumaliza pambano na yeye kupelekwa kwenye kona yake kwa msaada kabla ya kuanza kutapika hali iliyomfanya daktari wa pambano, Khadija Hamisi kuchukua uamuzi wa kumkimbiza hospitali kwa gari ya wagonjwa lililokuwepo uwanjani.

Kwa mujibu wa ripoti ya daktari huyo kwa sasa bondia huyo anaendelea vizuri.

“Tunashukuru anaendelea vizuri kwa sababu amepatiwa matibabu na hadi sasa bado anaendelea na matibabu lakini amefanikiwa kuamka na anaongea, alichokuwa analalamika ni maumivu ya kichwa ingawa alitapika.

“Lakini amepewa rufaa ya kwenda Hospitali ya Mwananyamala ambapo tutampeleka kwa ajili ya kufanya vipimo vya CT Scan kuangalia hali ya kichwa ipoje na vipimo ambavyo alifanya usiku baada ya kufika Temeke anaonekana yupo sawa isipokuwa hiyo CT Scan ambayo itafanyika leo,” alisema Dk Hadija.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live