Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ndondi Taifa warudia uwanja wa ndege

JNIA KENYA Timu ya Taifa ya Ndondi haijakwenda mashindanoni, yaishia JKIA

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Licha ya ratiba ya Shirikisho la ngumi za ridhaa la dunia (AIBA) kuonyesha bondia Alex Sulwa atapanda ulingoni jioni leo Oktoba 28 nchini Serbia kwenye mashindano ya dunia, msafara wa Tanzania umelazimika kugeuzia uwanja wa ndege jijini Nairobi na kurejea nchini.

Inaelezwa timu hiyo iliyokuwa na watu wanne ilalala uwanjani hapo kabla ya kurejea nchini na kukwama kushiriki kwenye mashindano hayo yanayoendelea katika mji wa Belgrade.

Ratiba ya AIBA inaonyesha Alex atacheza jioni ya leo katika raundi ya raundi ya pili dhidi y a Congo Gerlon wa Ecuador iliyopo pwani ya magharibi ya Amerika Kusini.

Hata hivyo bondia huyo na wenzake wamerejea nchini baada ya kukwama  kwenye uwanja wa ndege wa Nairobi huku Watanzania wengine, Michael Changarawe na Kassim Mbundwike wakionekana kupoteza kwa matokeo ya walkover.

Kwa mujibu wa AIBA, Alex kama angecheza leo na kushinda angefuzu kucheza robo fainali Jumapili na mshindi kati ya Mullojonov Lazizbek wa Uzbekistan ya jamhuri ya Asia ya Kati au Kim Do Hyeon wa Korea.

"Ni kweli tuliishia uwanja wa ndege baada ya kukosa visa, tulitarajia tuondoke jana lakini tulikwama na tayari baadhi yetu tuliondolewa mchezoni," amesema Changarawe.

Makamu wa rais wa TOC, Henry Tandau anasema wameshangazwa timu hiyo kutosafiri kwa kuwa waliisaidia na walitarajia wawe wameondoka.

"Tulipigiwa simu na wakala wa safari, akasema timu imefika uwanja wa ndege, lakini hawakuondoka hadi ndege ikawaacha.

"Tunachosikia ni kwamba walilala pale pale uwanjani, hivyo tunataka warudishe pesa ambayo TOC tuliwapa," amesema.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz